Balozi wa TZ hapa UK, Mh Mbelwa Kairuki (@MbelwaK) ajibu madai kwamba ubalozi huo unadaiwa sh bilioni 7.5 za maogesho, asema balozi zote hazipaswi kulipa kodi kwa mujibu wa Vienna Convention

habarimedia Avatar
Get more from Evarist Chahali in the Substack app
Available for iOS and Android

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki amejibu madai kuwa ubalozi huo unadaiwa shilingi bilioni 7.5 za maegesho jijini London.

Balozi Kairuki ameeleza yafuatayo

Jiji la London lilianzisha tozo ya maegesho (Congestion charge) kwa magari yanayoingia katikati ya jiji la London mwaka 2003.

Madai yaliyoorodheshwa kuhusu hilo linaloitwa “deni hilo kwa ubalozi” ni ya kuanzia wakati huo hadi leo (miaka 21) tofauti na ulivyodhani kama ni deni la karibuni.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa -Vienna Convention- Balozi hazipaswi kulipa kodi;

Ushauri wa kisheria (legal opinion) uliotolewa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) Sir Christopher Greenwood ulieleza kwamba hiyo tozo iliyoanzishwa mwaka 2003 ni KODI;

Huo ndio msingi wa nchi mbalimbali kutolipa kodi hiyo. Sio suala la kuwa na uwezo au kutokuwa na uwezo- ndio maana Balozi za nchi zinazodaiwa amount kubwa ya kodi hiyo ni Marekani inayodaiwa takriban Bilioni 46, ikufuatiwa na Japan na wengine.

Balozi Mbelwa alieleza kuwa taarifa za kutosha kuhusu suala hilo zipo hadharani (on public domain) na kuhamasisha wenye nia ya kufahamu zaidi kuhusu suala hilo wafanye utafiti japo kidogo.

Tagged in :

habarimedia Avatar