Tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Hanan Mohamed Bafagih, adaiwa kuhusika na kipigo cha kijana aliyeishia kupoteza nguvu za kiume

habarimedia Avatar
Get more from Evarist Chahali in the Substack app
Available for iOS and Android

Jasusi anawasilisha waraka husika kama alivyoupokea, hajaongeza wala kupunguza neno.

UKATILI WA MKURUGENZI WA WILAYA HALIMASHAURI WA

WILAYA KILWA – Hanan Mohamed Bafagih Aliyempiga kijana mpaka kumuondolea Nguvu za kiume.

Mambo kama ya Pauline Gekul yamejirudi huko Kilwa. Mateso kwa kijana Ahmed Selemani Kidagaa, amepigwa na usalama wa Taifa kwa Amri ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa akituhumiwa kuiba ndani ya nyumba ya Mkurugenzi huyo.

Taarifa za tukio hili ambazo ziko polisi ni hizi hapa chini zilizoandikwa na Afande.

AFANDE WAZIRI MKUU

1. Tarehe 30/01/2024, Majira Ya 1630 Hrs, Ulitumia Video Clip Ya Kijana Mmoja Mkazi Wa Wilaya Ya Kilwa Mkoani Lindi Akilalamika Kupigwa Na Polisi/Usalama wa Taifa

Alilazimishwa kukiri kuiba Fedha.

2. Nilifuatia Mara Moja Na Kubaini Kwamba Tarehe 18/09/2023 Nyumbani Kwa Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Kilwa Aitwaye Hanan D/O Mohamed Bafagih, 29 Yrs. Mzanzibar Muislamu Mkazi Wa Kilwa Masoko Kuliripotiwa Tukio La Wizi (Jalada Klm/Ir/523/2023 Lahusika).

3. Mkurugenzi Huyo Alikuwa Anaishi Nyumba Na Chumba Kimoja Na Rafiki Yake Wa Kike Aitwaye Fatuma D/O Ayubu Mandari, 36yrs. Mchaga, Muislamu, Psychologist Mkazi Wa Masoko Amba Ndiye Anayetunza Funguo Za Nyumba Na Funguo Za Chumba.

4. Katika Tukio Hilo Ziliibwa Fedha Taslim Sh.14,000,000/= Na Mikufu Miwili Ya Dhahabu Yenye Thamani Ya Sh. 10,000,000/= Hivyo Kufanya Thamani Ya Jumla Sh 24,000,000/=.

5. Baada Ya Tukio Hilo Walikamatwa Watuhumiwa Saba:-

Wilaya wakijaribu kumaliza ili suala na kijana, sababu Mkurugenzi alitesa kwa kutumia cheo, Mamlaka za wilaya na mkoa zimekuwa zikutumia nguvu kuzima ili suala

Kwa nini mamlaka zinataka kuzima hili suala?

Kuna Taarifa kwamba Hanan Mohamed Bafagih ambaye ni Mkurugenzi wa Kilwa na Mzanzibari anatamba hapo wilayani na mkoani kwamba wasipomaliza ili suala wao ndio watachukuliwa hatua sababu yeye ni mtoto wa kufikia wa Rais Samia Suluhu na ndiye aliyemsomesha, na wasijifanye hajui amefikiaje hapo.

Polisi wanaogopa hii kesi na mkuu wa wilaya anajaribu kumdanganya huyu kijana kumaliza ili suala, huyu kijana kabla ya kipigo alikuwa mzima wa afya, lakini sasa hana uwezo wa kushiriki tendo la ndoa na mkewe, kwa sababu tu amepewa tuhuma na mkurugenzi wa Halmashauri ambayo ni binti wa Rais.

Polisi mko wa Dar wanajua suala ili, kuna nguvu kubwa sana inatumiwa na Waziri kuhakikisha huyo mwanafamilia mwenzie anapona na kwenye hii kesi, Waziri mwenye dhamana naye ni mwanafamilia wa Rais Samia, kwa kifupi Kijana Ahmad anakosa haki yake sababu kwenye familia moja waliogawana madaraka wamemumiza

Ahmad kwenye video anaomba msaada kwa Rais Samia, lakini ukiangalia kwa uelewa suala ili linamuhusu Rais Samia, kijana wa watu yeye anaona kwamba labda Rais wa wananchi anaweza simamia haki yaki, lakini Mchengerwa ambaye ni Waziri wa TAMISEMI ndiye anayefanya juhudi kubwa sana kuzima ili suala chini kwa chini

Suala kubwa kwa Mchengerwa kama ndugu yake angefanyiwa hivi angekubali?

Kama mtu anatuhuma ya wizi mfumo wa sheria si upo tunambiwa kila siku fuata taratibu? Kwa nini wizi huu wameshikwa watu wengi na kutupia polisi kisha wote baada ya kuteshwa wakaachwa tu?

Kwa nini polisi wamekataa kijana huyu kuendelea na kesi? Kwa nini polisi wanaiogopa hii kesi kama sio mikono mikubwa ya wanafamilia hawa waliamua kupoteza haki ya kijana huyu?

Ni watanzania wangapi wataendelea kuteshwa namna hii? Hizo fedha milioni 14 mkurugenzi alikuwa nazo za nini wakati kila siku wanatuambia tutumie Bank?

Sheria za BoT zinasema nini kuhusu kubabe fedha Zaidi ya milioni 10? Mkurugenzi hajui hiyo sera ya

nchi kwamba fedha kwa kiasi hicho alitakiwa kuziweka bank au kuziweka mazingira salama?

Inakuaje Mkurugenzi anaweka kienyeji tu million 14 mpaka zinachukuliwa kirahi kama kweli tukio limetukea au anawazingizia tu?

TUNAOMBA UMMA KUMPIGANIA KIJANA AHMAD,

Tunakumbuka wote tukio la babati

TUSIKUBALI HAKI YA AHMAD KUPOTEA |

MENGINEYO

Tagged in :

habarimedia Avatar